Sunday, May 12, 2013

REDDS MISS KIBAHA 2013



KAMATI  ya Miss Tanzania ikiongozwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino International Agency, Hashim Lundenga  imewafunda ipasavyo warembo wanaoshiriki katika shindano la Redd’s Miss Kibaha 2013 litakalofanyika Mei 17 Ukumbi wa Container Mailimoja Kibaha, Pwani.

Akizungumza katika kambi ya warembo hao, Lundenga aliwataka wajijengee hali ya kujiamini na kila mshiriki asimwogope mwenzake na kila mmoja awe amejiwekea lengo la kufika katika shindano la kanda na hatimaye taifa.
Aidha, Lundenga amewaasa warembo hao kumpa sapoti mrembo atakayetwaa taji hilo.
“Endapo mrembo mwenzenu yeyote ataibuka na kutwaa taji, lazima mumpe sapoti kubwa, kwani ‘crown’ huvaliwa na mrembo mmoja tu, hivyo nawatakia kila la kheri katika shindano lenu na niwaahidi tutakuwa pamoja hadi siku ya shindano,” alisema.
Lundenda alionya kuwa mrembo atakayeonesha utovu wa nidhamu atatolewa katika shindano hata kama itakuwa ni siku ya fainali, hivyo amewataka wawe makini wakati wote.

Wakati huohuo, Miss Tanzania 2012 Briggite Alfred, aliyeambatana na kamati hiyo, alitumia fursa hiyo kuwatoa shaka ya mrembo kupangwa kuanzia katika ngazi ya awali hadi taifa.
“Warembo wenzangu, kwanza nawapongeza kwa hatua hii ya kujitosa kushiriki, kwani ni hatua kubwa, kwa sababu hata mimi nilianzia katika ngazi ya awali kama hii, lakini tangu nilipoingia katika shindano nilijiona ni mshindi hali iliyonijengea kujiamini hata nilipokwenda katika shindano la kanda na hatimaye taifa, hivyo nawatakia kila la kheri,” alisema.
Shindano hilo linaloandaliwa na Kampuni ya Linda Media Solution litapambwa na bendi ya Mashujaa ‘Wana Kibega’ huku kiingilio kikiwa sh 10,000 kwa VIP na viti vya kawaida sh 6,000.

Limedhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania kwa kupitia kinywaji chake cha Redds Premium Cold, Shear Illusions, Fredito Entertainment, CXC Africa, Multichoice DSTV, Times FM, Michuzi Media Group (MMG), Santorine Holiday Resort, PR. Promotion, Aco Catering Servises, Amazon Night Club na  Panandipanandi Pub.

No comments:

Post a Comment