Sunday, May 12, 2013

Mitindo rahisi ya nywele ya kuchana nyumbani



NYWELE na mitindo yake ni kitu kinachowagharimu sana wanawake, hasa katika matumizi ya fedha na muda.

Hali hiyo hufanya wengi kutafuta mitindo ambayo itakaa kichwani muda mrefu bila kwenda saluni ama bila kuchana nywele nyumbani, kwani huwa ni vigumu, mtindo wa nywele hasa ule wa mara moja kuweza kuurudia uwapo nyumbani ama asubuhi wakati wa kwenda kazini.



Kuna mitindo mingi ya kujitengeneza nyumbani bila kwenda saluni, ukarekebisha nywele zako na ukaoneka mtanashati.

Kwa wale wenye nywele ndefu, chana nywele vizuri na zivute sana, halafu zikusanye kabla ya kufika kisogoni kisha unaweza kuzibania hapo au ukazivutia kwa pembeni na ukabana pia.

Ni vyema kama utabana na kibanio chenye  extension kwani hiki husaidia kuzishika nywele ipasavyo, na kuondoa kuvurugika nywele haraka.

Hakikisha una vifaa vyote vya nywele ikiwa ni pamoja na vitana vya aina zote, shampoo kwa kuosha nywele inapobidi kufanya hivyo nyumbani, mafuta ya nywele, spray, pink losheni, conditioner nakadhalika, ili kukupa urahisi pale unapofikiria mtindo wa haraka wa kutengeneza nyumbani.

a nywele fupi ambazo zina dawa, hakikisha umeweka mawimbi mazito, na wakati wa kuchana chukua kitana chenye meno makubwa yaliyoachana kisha chana kwa kufuata upande, aidha kama unataka mtindo wa pembeni chana kwa kufuata upande wa kushoto au kulia, chana kwa kuchambua ili yasiharibike.

pia unaweza kuchana nywele kwa kitana kikubwa kabisa, bila kuzilaza na kuzivuta kwa nyuma kwa kuzigawanya, utapa mtindo rahisi na wa kupendeza.


Kwa waliosuka 'wiving' chukua kitana maalum kwa ajili ya wiving, kisha chambua mstari mmoja, chana, pitia wa pili mpaka utakapomaliza, kisha changanya kwa kuchana nywele zote na zibane kama ni ndefu.


Kumbuka hii ni mitindo myepesi ya kuchana uwapo nyumbani bila kwenda saluni, na ukimaliza kutengeneza nywele ni vyema ukazinakshi kwa spray kwa ajili ya kuzifanya zing'ae na zenye kupendeza.

No comments:

Post a Comment