Monday, May 13, 2013

Matatu ya Somalia yagoma



 Waendesha mabasi nchini Somalia wamegoma kwa siku ya pili kwa sababu wanasema inabidi wawalipe rushwa wanajeshi wa serikali na polisi katika vituo vya ukaguzi.
Mkaazi wa Mogadishu atumia baiskeli badala ya basi
Madereva wa mabasi na malori mjini Mogadishu na miji mengine wamekataa kufanya kazi hadi swala hilo limeshughulikiwa.
Kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini Somalia, AMISOM, kimeingilia kati kujaribu kutatua mkwamo huo.
Msemaji wa polisi ameiambia BBC kwamba wanachunguza malalamiko hayo lakini hawana habari kwamba askari polisi wanadai hongo.

No comments:

Post a Comment